Saturday, August 2, 2014

RUDISHA WA KENYA AAMBULIA FEDHA HUKO GLASGOW

Rudisha alikuwa bingwa wa Olimpiki mjini London mwaka 2012.
Nigel Amos ana miaka 20.
BINGWA wa Olimpiki na ambaye pia anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 800 mkenya David Rudisha aliambulia medali ya fedhakatika mashindano ya Jumuiya ya madola.
Hii ni baada ya kushindwa na mshindani wake wa karibu Nijel Amos mwenye umri wa miaka 20 katika mashindano hayo yanayoendelea mjini Glasgow Scotland.
Amos, ambaye alishinda medali ya fedha katika mashindano ya olimpiki mjini London alimaliza mbio hizo kwa kishindo baada ya kutoka nyuma ya Rudisha na kumpiku.
Kwa kawaida, Rudisha alikuwa mbele wakati wa mbio hizo kwa mita 150 na kudhibiti mbio zenyewe kama alivyofanya alipovunja rekodi mwaka 2012.
Lakini alikiri kuwa mbio hizo hazikuwa ngumu , ila mita miamoja za mwisho ndizo zilizomtatiza na hapo ndipo Amos aliweza kumpiku Rudisha.
 Baada ya kupata jeraha baya la goti mwaka 2013, Rudisha amekuwa mbioni kuuguza jeraha lake na pia umekuwa wakati mgumu wake kwani washindani wake wamekuwa pia wakifanya mazoezi wakilenga kumshinda.
Alionekana kuishiwa na nguvu wakati Amos kutoka Botswana alipompiku na kuanza kusherehekea na kushinda dhahabu.
Rudisha mwenye umri wa miaka 25 alimaliza mbio hizo kwa dakika 1:45.48 nyuma ya Amos huku Andre Olivier wa Afrika Kusini akinyakua Shaba.
Amos aliambia BBC kuwa ana raha sana ingawa Rudisha daima atasalia kuwa bingwa wa mbio za miata 800.
Mbio hizo zilikuwa moja ya mbio zilizosubiriwa kwa hamu kuu katika mashindano hayo ya Jumuiya ya madola.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI