Na Mahmoud Ahmad, Monduli
JAMII ya kifugaji nchini bado inakabiliwa na changamoto ya kuficha watoto walemavu hali ambayo nikinyume cha haki za kibinadamu na haki ya msingi ya mtoto na kumnyima fursa za kupata elimu na kujikwamua na kupambana na adui ujinga.
Hayo yalisemwa mapema jana na Diwani wa kata ya meserani Ew.Edward Laize akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ta mtoto wa Afrika mabayo huadhimishwa Juni 16 kila mwaka ambayo mwaka huu kauli mbiu yake ni kupata elimu bora na isiyo nakikwazo ni haki ya kila mtoto na maadhimisha hayo yalifanyika jana katika kata ya meseran katika shule ya shule ya msingi meserani chini iliyopo katika wilaya ya monduli mkoani arusha.
Hata hivyo alisema kuwa hali hiyo imetokana na baadhi ya mila ya jamii za kifugaji kuona kuwa na mtoto mlemavu nia aibu sana na pia nimkosi katika familia hali mabayo ikitokea kuzaliwa mtoto mlemavu kumficha ndani nahata baadhi ya familia nyingine za jamii hiyo kuweza kuua na kuficha aibu ya mtoto huyo badala yake aliwataka kubadili mtazamo huo nakuona watoto wote nisawa kama ambao hawanba ulemavu.
Aidha aliitaka jamii hiyo kuweza kushirikiana najamii inayowazunguka kuweza kufichua jamii inayofanya vitendo hivyo nakutoa taarifa katika vyombo vya dola ili sheria iweze kuchukua mkondo wake na kuweza kukomesha vitendo hivyo vya kuficha watoto hao.
Diwani Edward aliitaka Serikali kushirikiana na wadau mbalimbali wa haki za binadamu kuweza kuweka mikakati kuanzia ngazi ya hospitali nakuweza kufuatilia mtoto kama atazaliwa mlemavu ili kujua maendeleo yake ili kuweza kujua namna ya kuwasaidia watoto hao.
Kwa niaba ya watoto wenzake Innocent Herman darasa la tano katika shule ya msingi Meserani katika risala yao alisema kuwa watoto bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hali inayowapelekea kuacha shule ambapo miundombinu kutokuwa rafiki kwa watoto,kufanyishwa kazi za shuruba ,na umbali washule na makazi wanayoishi sambamba na uhaba wa walimu.
Aliongeza kuwa aliitaka Serikali kuweza kuondoa mila potofu kwa watoto ikiwemo ukeketaji ,ndoa za utotoni nakutopewa haki ya elimu bora na kulindwa badala yake wabadili mtazamo nakuweza kuwaondoa kweny vikwazo ili kuweza kupambana na adui ujinga na umasikini kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya monduli Bi,Rose Mhina alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya ongezeko la idadi ya watoto wnaoishi katika mazingira magumu niwengi na ukilinganisha na uwezo wa fedha za halmashauri amabpo watoto zaidi ya 5843 wanaishi katika mazingira magumu nahatarishi ,hali ambayo inawalazimu kusaidia watoto wachache kwa kuwalipia ada na wengine kuweza kusaidiwa na mashirika mbalimbali ambapo mwaka huu pesaa iliyoptengwa nish.milioni 7 pekee mabazo hazitoshi kumudu kulipa ada za watoto wote.
Aliwaomba Serikali kwa kushirikiana na wadau wa elimu kuweza kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuwasaidi watoto hao ili kuwapatia mahitaji muhimu hususani elimu na malazi ili kuweza kuwakwamua katika mazingira hayo na kuwapatia elimu ambayo ni haki yao ya msingi.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka shirika lisilo la kiserikali la World Vision Bw.Stey Steven aliwataka jamii ya kifugaji kuweza kujitokeza kwa kupeleka watoto shule na endapo familia haina uwezo wao wanawasaidia watoto kuwapa elimu kuanzia awali hadi chuo kikuu na uhitaji na ukomo wa mahitaji ya mwanafunzi husika.
0 comments:
Post a Comment