WEMA Sepetu ameonekana kufungukia wale wanaomtukana kila siku na sasa kufikia hatua ya kumtukana hadi mama yake mzazi...Kupita mtandao mmoja wa kijamii, Picha moja ya mama mzazi wa Wema Sepetu iliyotengenezwa na kuwa CHAFU ilitolewa na kisha kuanza kushushiwa matusi mazito...
Baada ya Picha na Matusi hayo, Wema amefunguka kwa uchungu kwa kuandika:
"Dah...! Sijui hata niseme nini...! Ila si mlitaka kuniumiza... leo mmefanikiwa... nawapeni hongera.... Tena mmetisha haswa... Kila siku huwa hata siumizwi na matusi yenu cuz naonaga kama ni mnajisumbua tu…
Hakuna siku nimelia kwa uchungu kama leo…
"I min mnitukane mimi mpaka mchoke but leave my mum out of it... Kawakosea nini nyinyi mama angu mpaka mfanye hivyo... Mzazi nwenyewe ndo nimebakia nae mmoja tu... mnataka afe na yeye nibaki yatima sio... dah... leo mmeniweza... saana jamani... Basi naomba isifike huko... nina uchungu sana na mama angu ... nampenda sana mama angu ila naona mnataka kuniulia mama angu…
"Picha halisi ndo hio hapo juu kweli mtu uende ukamfanyie hivyo mama wa mwenzako... una mama wewe.. au uliokotwa na hujui uchungu wa mama... dah... nime surrender leo.... hongera zenu narudia tena... mmeniweza leo.... dah…
"Mungu nipe nguvu ktk hili jamani... Kwani nilichokikosea haswa ni kitu gani mpaka iwe hivi . Nimekosa nini mimi yarabi toba.... Eeeh mungu... Dah... Ila nashkuru..." Ameandika Wema Sepetu kwa Uchungu
0 comments:
Post a Comment