Sunday, June 1, 2014

BAO PEKEE LA MASSA LAWAVUSHA UGANDA HATUA INAYOFUATA, RWANDA YAIKANYAGA LIBYA 3-0

UGANDA The Cranes imefanikiwa kusonga hatua inayofuata katika michuano ya kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika, AFCON 2015 nchini Morocco baada ya kufanikiwa kuiondosha Madagascar kwa wastani wa mabao 2-2, lakini Uganda wamenufaika kwa faida ya bao la ugenini.
Uganda jioni hii wameibuka na ushindi wa bao 1-0 mjini Kampala katika mchezo wa marudiano, na mechi ya kwanza walilala kwa mabao 2-1 nchini Madagascar.
Bao pekee la Uganda limefungwa na Geoffrey Massa katika dakika ya 12 ya kipindi cha kwanza na kuwasimamisha vitini mashabiki waliofurika kuitazama timu yao.
Katika mchezo mwingine uliomalizika jioni hii, timu ya taifa ya Rwanda ``Amavubi` imefanikiwa kusonga mbele kwa wastani wa mabao 3-0 kutokana na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Libya walioupata jioni hii.
Mabao yote ya Rwanda yamefungwa na Dady Birori katika dakika ya 39`, 64 na 72.
Mechi ya kwanza Rwanda walitoka suluhu ya bila kufungana na Libya mjini Tripoli.
Mechi nyingine zinazopigwa leo ni baina ya Guines Bissau dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya kati, wakati nao Sierra Leone watachuana na Swaziland.
Mechi baina ya Seychelles dhidi ya Gambia imeahirishwa.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI