Tuesday, May 20, 2014

WAKAZI WA JIJI LA DAR WAUNGANA NA MKUU WA MKOA, NA MEYA WA KINONDONI KUFANYA USAFI MTO MLALAKUWA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akiungana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda walipoungana na wananchi kufanya usafi katika mto wa Mlalakuwa jijini Dar es Salaam ili kuepukana na ugonjwa uliozuka wa Dengue ambao umekuwa tishio wakati akizindua zoezi la kufanya usafi jijini lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda pamoja na wananchi walioungana nae, wakiangalia jinsi mto Mlalakuwa ulivyoharibiwa kutokana na mvua zinazoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (mbele) akiongozana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda kuvuka Mto Mlalakuwa kuongea na wananchi waliokuwa ng'ambo ya mto.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akiwahimiza kuhama wananchi wanaoishi pembezoni wa Mto Mlalakuwa kutokana na nyumba yao kubomoka na maji kama inavyoonekana.
Zoezi la usafi halikujali rangi wala taifa..
Mto Mlalakuwa ukiwa safi mara baada ya zoezi kumalizika.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI