MKUU wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifungua rasmi mkutano wa wadau wa uhamasishaji wa ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi PPP - ("Public and Private Partnership") katika Sekta ya Afya uliofanyika leo katika ukumbi wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa.
Katika hotuba yake ya ufunguzi amesema ili kufikia lengo kuu la millennia ifikapo mwaka 2015 la kupunguza vifo vya watoto, akina mama wajawazito na kuweza kudhibiti magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza pamoja na kuboresha mazingira na kupata maji salama Serikali peke yake haitaweza bila kushirikiana na Sekta Binafsi ambayo pia imekua na mchango mkubwa katika kujenga afya za watanzani.
Ndugu Paul Michael Nadrie muwezeshaji wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi PPP - (Public and Private Partnership) katika Sekta ya Afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akiwasilisha moja ya mada katika Mkutano huo. Alieleza kuwa zipo faida nyingi za PPP ikiwemo kuongeza na kusogeza huduma za afya kwa wananchi pamoja na kuongeza ushindani katika kutoa huduma za afya nchini.
Akigusia changamoto amesema zipo changamoto nyingi ikiwemo uelewa hafifu wa PPP kwa watekelezaji na jamii kwa ujumla, uwazi katika utekelezaji wa PPP (Public and Private Partnership), upatikanaji wa mikopo ya mda mrefu, uwezo hafifu wa kufanya upembuzi yakinifu na uwezo hafifu wa kiuchumi katika kushiriki kwenye miradi ya PPP (Public and Private Partnership).
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akitambulisha wajumbe katika kikao hicho kutoka Sekta Binafsi na Sekta ya Umma. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com.
0 comments:
Post a Comment