Mbunge
wa Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), akizungumza na viongozi wa
Mahakama ya Qadhi wakati alipotembelea Mahakama hiyo kuona namna
inavyohudumia waumini wa Dini ya Kiislamu katika kutatua migogoro ya
ndoa.
Sheikh
wa Mahakama ya Qadhi, Ramadhani Kaoja akimweleza Mheshimiwa Mbunge
shughuli za Mahakama hiyo pamoja na changamoto mbalimbali
zinazowakabili, Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Singida Mjini , Hamis
Nguli, wa pili kulia ni Katibu wa Mahakama ya Qadhi, Alhajj B. Mlau.
Mbunge
wa jimbo la Singida Mjini MO akisalimiana na waumini wa Msikiti wa Kata
ya Mtipa wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Msikiti huo,
ambapo mara baada ya kuona hatua zilizofikia za ujenzi huo aliahidi
kutoa Mabati 50 pamoja na mifuko 50 ya Saraji kwa ajili ya kukamilisha
ujenzi huo.
MO akitoka kukagua ujenzi wa Msikiti wa kijiji cha Mangwanjuki kata ya Mtipa.
Waumini wa Msikiti wa kijiji ch Mangwanjuki wakimsikiliza Mbunge wao Mheshimiwa MO.
Baadhi ya wapiga kura wa kijiji cha Mangwanjuki wakipeana mikono ya Kheri na Mbunge wao.
Baadhi
ya waumini wa dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Mwankonko darajani
wakimsikiliza Mbunge wao (hayupo pichani) wakati alipoendelea na zoezi
la kutembelea nyumba za kuabudu zilizopo jimboni kwake.
Jengo
la wa Mwankonko darajani likiwa kwenye hatua Lenta, ambapo baada ya
Mbunge kuona hatua hiyo ya nguvu za wananchi aliahidi Bati 50 na Mifuko
ya Saruji 50.
Mheshimiwa Mohammed Dewji na baaadhi ya viongozi wa Msikiti wa kijiji cha Kisasida.
Mbunge
MO akizungumza na waumini wa Msikiti wa Kisasida, ambapo ameahidi kutoa
msaada wa Mabati 100 na Mbao 100 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa
Msikiti huo.
MNEC
wa Manispaa ya Singida, Hassan Mazala akitoa hamasa kwa wakazi wa
Kisasida kushiriki Mkutano wa hadhara ambao umeitishwa kwa ajili ya
Katibu Mkuu CCM Taifa, Abdulrahman Kinana wa kuongea na wakazi wa jimbo
la Singida Mjini utakaofanyika viwanja vya People’s Club.
Mheshimiwa Mohammed Dewji akielekea kukagua ujenzi wa Msikiti wa Minga mjini Singida.
Watoto
wa Madrasa ya Msikiti wa Mwankoko Darajani wakimpokea Mbunge wao kwa
mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati alipotembelea ujenzi wa Msikiti
huo.
Mheshimiwa Mohammed Dewji akifurahia jumbe zilizoandikwa na watoto wa Madrasa ya Mskiti wa Mwankoko Darajani.
0 comments:
Post a Comment