Serikali imesema kuwa Sudan
sio nchi ya kwanza kutekeleza
sheria za kiisilamu
MAHAKAMA nchini Sudan imemhukumu
kifo mwanamke mmoja anayedaiwa kubadili dini
yake na kuolewa na mwanamume mkristo.
Daktari Mariam Yahya Ibrahim Ishag, ambaye babake
ni muisilamu alishitakiwa kwa kosa la kuasi dini
pamoja na kufanya zinaa kwa kuolewa na
mwanamume mkristo , kitu ambacho dini ya
kiisilamu imeharamisha kwa wanawake.
Sudan…!
Mariam mwenye umri wa miaka 28 pia ni mjamzito
na ataadhabiwa kwa kuchapwa mijeledi miamoja
kwa kosa la zinaa.
Maafisa wakuu wanasema kuwa licha ya
Mariam kulelewa kwa njia ya kikristo yeye bado
ni muisilamu kwa sababu hiyo ndiyo dini ya babake.
Alipewa siku tatu baada ya kuhukumiwa aweze
kurejea katika dini ya kiisilamu lakini akakataa na
ndio maana adhabu ikasalia.
Kwa kawaida wanawake waisilamu
hawaruhusiwi kuolewa na wanaume wakristo
ingawa wanaume waisilamu wanaruhusiwa
kuwaoa wanawake wakristo.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za
binadamu Amnesty International linasema kuwa
Bi Ishag alilelewa kama Mkristo muorthodoxi
kwa sababu babake hakuwepo naye maishani mwake.
'Kesi ya kwanza'
Kesi ya Ibrahim ni ya kwanza ya aina yake
kusikika nchini Sudan , kwa mujibu wa shirika la
habari la Reuters.
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu,
wamelaani uamuzi huo wa mahakama na
kuitaka serikali ya Sudan kuheshimu haki na uhuru
wa watu kuabudu.
Maafisa wa balozi za mataifa ya magharibi
pia wamekemea vikali kesi hiyo na kuelezea asiwasi
wao kuihusu.
Maafisa hao wamewataka maafisa wa sheria
nchini humo kuangalia kesi hiyo upya na
kuhakikisha kuwa Mariam anatendewa haki.
Waziri wa mawasiliano amesema kuwa sio Sudan
peke yake ambako sheria za kiisilamu zinafuatwa
na ambako sio sawa kwa mtu kubadili dini yake,
hali hiyo pia ipo nchini Saudi Arabia na katika
nchi zingine zinazofuata sheria za kiisilamu.
Serikali ya Rais Omar al-Bashir inakabiliwa
na changamoto nyingi za kiuchumi na kisiasa hasa
baada ya kujitenga na Sudan Kusini ambako
mafuta yake yalikuwa yanatoka mwaka 2011
|
0 comments:
Post a Comment