Tuesday, April 1, 2014

TEKNOLOJIA YAPELEKA SHULE YA MSINGI KANING’OMBE, IRINGA

Kiswaga akimkabidhi kompyuta mkuu wa shule ya Kaning’ombe Bw Mohamed Mchamba (kushoto)
Viongozi wakifurahia msaada huo
Na Francis Godwin Blog
MDAU wa maendeleo katika jimbo la Kalenga mkoani Iringa Jackson Kiswaga ambae ni mkazi wa kijiji cha Nyamihuu amezidi kusaidia maendeleo ya wakazi wa jimbo la Kalenga kwa kukabidhi msaada wa kompyuta na printa katika shule ya msingi Kaning’ombe.
Msaada huo umetolewa jana na Kiswaga kama utekelezaji wa maombi ya wazazi na uongozi wa shule hiyo ambao mwaka jana wakati wa mahafali walimwombe kuwasaidia vifaa hivyo ili kusaidia kuchapa na kuprinti mitihani ya wanafunzi shuleni hapo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Kiswaga alisema kuwa furaha yake kuona wanafunzi shuleni hapo wanajifunza komyupta na uongozi wa shule hiyo unapata kitendea kazi kwa ajili ya kufanyia kazi za wanafunzi.
Kwani alisema kuwa kompyuta hiyo itawasaidia kuchapa mitihani ya wanafunzi na kuondoa kero kubwa ambayo walikuwa wakiipata awali kwa kusafiri zaidi ya km 30 kwenda mjini Iringa kuchapa mitihani ya wanafunzi.
Hata hivyo Kiswaga alisema kwa kuwa eneo hilo hakuna umeme na kifaa hicho kinahitaji umeme atawasaidia msaada wa genereta kwa ajili ya kusaidia umeme katika utumiaji wa kompyuta hiyo. 
Pia alisema akiwa kama mdau wa maendeleo katika jimbo hilo ataakikisha aaendelea kusaidia pale ambapo atakuwa na uwezo napo huku kuhusu maombi ya wananchi hao kufikishiwa huduma ya mtandao wa simu kwa kufungiwa mnala wa tigo alisema kuwa mambi hayo atayafikisha kwa viongozi wake wa juu ili kuangalia uwezekano wa kusaidia japo alisema hawezi wadanganya kuwa atafikisha mnala huo kesho .
Mkuu wa shule hiyo Mohamed Mchamba mbali ya kumshukuru Kiswaga kwa msaada huo bado alisema kuwa jitihada kubwa zinazofanywa na mdau huyo ni ukombozi katika sekta ya elimu shuleni hapo.
Kwani alisema kuwa shule hiyo toka ilipoanzishwa haijapata kuwa na kompyuta hivyo msaada huo ni mkubwa kwao na kuomba wadau wengine kuzidi kusaidia shule hiyo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI