Mwanafunzi wa Eden Hilling College aliyetajwa kwa jina la Atu Gabriel amefariki akidaiwa kujaribu kutoa mimba kwa kunywa vidonge.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani (RPC), Orech Mtei, katika kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, alisema Jumamosi April 26 mwili wa Atu ulikutwa katika chumba cha mwanaume aliyefahamika kwa jina la Hafidhi ambaye anadaiwa kuwa mpenzi wake.Kamanda Mtei ameeleza kuwa polisi walikuta mwili wa marehemu ukiwa karibu na vidonge alivyotumia huku akitokwa damu nyingi sehemu za siri na kwamba polisi wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa Hafidhi ambaye alidaiwa kukimbia baada ya tukio."Ni kweli tukio hilo limetokea Jumamosi Aprili 26 mwaka huu eneo la Kwa Mfipa baada ya jeshi letu kutaarifiwa kuwepo kwa mwili huo na polisi walipofika na kufanya uchunguzi wake tulibaini marehemu alifariki dunia kaika jaribia la utoaji wa mimba.....hata hivyo mwili bado upo Hospitalini Tumbi kwa ajili ya uchunguzi zaidi," alisema Kamanda Mtei.
Kamanda Mtei alisema mara baada ya kutokea kwa tukio hilo, kijana aliyetajwa kwa jina la hafidhi ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake alitokewa eneo la tukio na jeshi hilo kwa sasa linamtafuta kwa ajili ya mahojiano zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani.
"Baada ya tukio mtuhumiwa alikimbia na hadi sasa bado haijulikana alipo, jeshi letu linaendelea kumtafuta popote alipo na mara baada ya kumpata tutamuhoji na baadae atafikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua za kisheri," alisema Mtei.
Secretary wa Eden Hilling College ambaye hakutaka jina lake litajwe alieleza kuwa mwanafunzi huyo aliaga chuoni hapo siku ya Alhamisi kuwa anakwenda katika hospitali ya Mwananyamala kumuuguza wifi yake na kwamba wamesikitishwa sana na habari ya kifo cha mwanafunzi huyo.
"Aliaga vizuri tu siku ya Alhamisi kwamba anauguliwa na anakwenda kumuuguza wifi yake aliyelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala lakini Jumamosi ndio tukapokea taarifa za kifo chake! Hii inaonyesha huyu mwanafunzi aliudanganya uongozi wa Chuo kitu ambacho hakikuwa sawa kabisa," Alisema.
Alisema hivi sasa uongozi wa Chuo unawasiliana na wazazi wake waliopo Makambaku kwa ajili ya kuja kuuchukuwa mwili wa marehemu.
Kwa undani wa habari hii na kusikiliza alichokisema RPC wa Pwani, ndugu na jamaa wa marehemu na majirani katika nyumba aliyokutwa wakisimulia tukio hilo, usikose kusikiliza Hatua Tatu ya 100.5 Times Fm Leo (April 28) katika kipengele cha Habari Ndio Hiyo na Maryam Kitosi, Edson Mkisi Jr na Dj R Guy.
Kipindi cha Hatua Tatu kinakuwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa sita kamili na Maryam Kitosi, Edson Mkisi Jr. na Dj R Guy.
0 comments:
Post a Comment