KATIBU Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana ameingilia kati Mgogoro wa ardhi uliokuwa ukifukuta kwa muda mrefu katika kijiji cha Mawenzusi katika wilaya ya Sumbawanga.
Mgogoro huo ulihusu Wananchi na anayedaiwa kuwa Mwekezaji, inaelezwa kuwa maamuzi yalikwishatolewa na Mh. Rais Jakaya Kikwete kuwa Wananchi wapewe kipaumbele na Mwekezaji apewe kiasi, lakini mpaka sasa hakuna lililotekelezwa kufuatia Watendaji waliokuwa wamepewa dhamana ya kulisimamia jambo hilo kusuasua na hatimaye kutopatiwa ufumbuzi wa haraka.
Kinana yuko mkoani humo kwa ziara ya siku sita ya kuangalia uhai chama, miradi na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi.
Fuatilia kwa makini video hapa chini:
Fuatilia kwa makini video hapa chini:
0 comments:
Post a Comment