Saturday, March 29, 2014

YANGA KAMILI GADO TANGA, WAANZA KUTUPA NDOANA KUWAVUA MGAMBO KESHO

Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezni jana jioni katika Viwanja vya shule ya sekondari Loyola
Kikosi cha timu ya Young Africans tayari kimeshawasili salama jijini Tanga jana mchana kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya maafande wa Mgambo JKT utakaopigwa siku ya jumapili katika dimba la Uwanja wa Mkwakwani na jioni ya leo timu imefanya mazoezi katika Uwanja wa shule ya Sekondari Galanos eneo la Nguvumali.
Young Africans ambayo katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya timu ya Tanzania Prisons iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 5-0, wachezaji wake wlikua wachangamfu sana mazoezini leo kila mmoja akisema wanapigana kutetea Ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo.
Kocha Mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van der Pluijm amesema vijana wake wanaonekana kumuelewa vizuri sasa na kuyashika vilivyo mafunzo yake na ndio maana matunda yameanza kuonekana katika michezo miwili iliyopita kwa timu kuweza kujikusanyia pointi 6 na magoli nane ya kufunga, huku safu ya ulinzi ikizuia timu pinzani kuziona nyavu zao.
Msafara wa watu 29 umefikia katika hoteli ya Central iliyopo barabara ya nane jijini Tanga ambapo ndipo Young Africans hufikia pindi inakua na michezo ya Ligi Kuu.
Wachezaji waliopo jijini Tanga ni :
Magolikipa: Juma Kaseja na Ally Mustafa "Barthez"
Walinzi: Mbuyu Twite, Juma Abdul, Oscar Joshua, David Luhende, Kelvin Yondani na Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Frank Domayo, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Nizar Khalfani na Athuman Idd "Chuji"
Washambuliaji: Emmanuel Okwi, Mrisho Ngasa, Saimon Msuva, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete, Hamisi Kizza na Hussein Javu 

Chanzo: Tovuti ya Yanga

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI