Mwenyekiti wa Wabunge wanawake Anna Abdallah (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wabunge wanawake Dkt. Mary Mwanjelwa (kushoto) wakibadilishana mawazo mjini Dodoma wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wanawake wa Bunge la Katiba ili kujenga muafaka wa agenda muhimu kwa maswala ya kijinsia.
(Picha na Tiganya Vincent - Dodoma)
Makamu Mwenyekiti wa Wabunge wanawake Suzan Lyimo akitoa mada mjini Dodoma kwa wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba kuhusu uwakilishi wa wanawake katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na umuhimu wa kuwa kitu kimoja katika kujadilia masuala ya wanawake katika Bunge Maalum la Katiba
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania(TGNP) Usu Mallya akitoa mada mjini Dodoma kwa wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba kuhusu uzingatiaji masuala ya haki za wanawake , utu na hali ya maisha na mgawanyiko wa raslimali wakati wa uandishi wa Katiba mpya.Mtoa mada kutoka TAWLA Victoria Mandari akitoa mada mjini Dodoma kwa wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba kuhusu umuhimu wa kuzingatia masuala ya mirathi na ndoa katika uandishi wa Katiba mpya.Baadhi ya wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa semina ya kuwajengea uwezo ili wasaidie kutetea kuingizwa kwa vifungu mbalimbali katika Katiba inayotarajiwa kuandika vinavyopinga unyanyasaji wa kijinisia.
0 comments:
Post a Comment