Mafunzo juu sheria ndogo ya mfuko wa afya ya jamii (CHF) ktk Halmashauri hiyo mpya
Viongozi wa Halmashauri ya Nyasa mkoani Ruvuma wakiwa katika mafunzo
Viongozi wa Halmashauri ya Nyasa mkoani Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa mfuko wa Taifa wa bima ya Afya (CHIF) ambao walitembelea Halmashauri hiyo kutoa mafunzo juu sheria ndogo ya mfuko wa afya ya jamii (CHF) ktk Halmashauri hiyo mpya
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu
Na Francis Godwin Blog, Nyasa
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amewataka viongozi wa Halmashauri ya Nyasa mkoani humo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ktk Halmashauri hiyo mpya
Mkuu huyo wa mkoa alitoa rai hiyo wakati wa warsha ya Viongozi wa Halmashauri ya Nyasa mkoani Ruvuma pamoja na watumishi wa mfuko wa Taifa wa bima ya Afya (CHIF)
ambao walitembelea Halmashauri hiyo kutoa mafunzo juu sheria ndogo
ya mfuko wa afya ya jamii (CHF) ktk Halmashauri hiyo mpya.
Alisema kuwa CHF ni Mfuko wa Afya ya Jamii, ulioanzishwa kisheria kupitia Sheria Na 1 ya mwaka 2001 (SURA 409 ya Sheria za Tanzania) ili kutoa huduma za matibabu kwa jamii iliyopo katika sekta isiyo rasmi mijini na hasa vijijini katika ngazi ya halmashauri, tarafa kata na kijiji hivyo iwapo viongozi hao watahamasisha jamii kujiunga ni wazi jamii hiyo itanufaika na huduma hiyo.
Hata hivyo alisema kuwa kujiunga na huduma hiyo ni utaratibu wa hiari unaoiwezesha kaya kupata huduma za matibabu kwa mwaka mzima kwa kuchangia mara tu kiasi cha shilingi 5,000/= au 10,000/= kwa kadiri jamii yenyewe katika Halmashauri husika itakavyoamua hivyo ni jambo zuri ambalo wananchi watanufaika nalo iwapo watajiunga .
Mwambungu alisema kuwa Serikali kwa upande wake inachangia kwa kiwango ambacho kaya inachangia hivyo kuufanya Mfuko huu kujulikana pia kwa jina la Tele kwa Tele.
“Mfuko huu ulianza kwa majaribio wilayani Igunga mwaka 1996 na baadaye kuenea katika Halmashauri mbalimbali nchini ijapokuwa kasi yake imekuwa sio ya kuridhisha. ….Mwaka 2007 Serikali iliamua kuwa Shughuli za Mfuko huu na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ziwianishwe…..
hatua hii ilisababisha Serikali kuu mwezi Juni 2009 kukasimu mamlaka yake kitaifa ya kusimamia na kuendesha CHF kuwa chini ya NHIF wakati Halmashauri zikiendelea na majukumu yake ya awali”
0 comments:
Post a Comment