TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
SERIKALI
imetangaza hatua kubwa na kabambe za kufufua usafiri wa abiria na
mizigo, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mabehewa na
injini za treni, katika hatua kubwa za aina yake kuchukuliwa na Serikali
kwa
muda mrefu katika kurekebisha usafiri wa treni nchini.
Waziri
wa Uchukuzi, Mheshimiwa Harrison George Mwakyembe ametangaza hatua hizo
leo,
Alhamisi, Januari 10, 2013, wakati alipokuwa anamkaribisha Rais wa
Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuweka jiwe la
msingi
kwenye ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Ndege wa Tabora ikiwa ni tukio la
mwisho
la ziara yenye mafanikio makubwa ya siku tano ya Rais Kikwete katika
Mkoa wa
Tabora.
Mheshimiwa
Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete na mamia kwa mamia ya wananchi
waliohudhuria
sherehe ya uwekaji jiwe hilo la msingi kwenye Uwanja huo kuwa Wizara
yake
imeanza kubadilisha reli nyepesi, iliyochakaa na yenye uzito mdogo kwa
Reli ya
Kati.
Amesema
kuwa kwa kupitia mashirika yake ya RAHCO na Shirika la Reli Tanzania
(TRL)
Serikali itafanya marekebisho hayo makubwa njia mzima ya Reli ya kati na
kuwa
mafundi wa mashirika hayo tayari wamefika Mkoa wa Morogoro.
Waziri
Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete kuwa Serikali kupitia Wizara yake na
mashirika yake hayo, imeagiza mabehewa mapya ya mizigo 274, imeagiza
mabehewa
mapya ya abiria 22, imeagiza mabehewa mapya ya kubebea kokoto 25 na pia
imeagiza mabehewa ya breki (brake vans) 34 na tayari malipo ya awali
yamefanyika.
Katika
namna inayothibitisha dhamira ya Serikali kurekebisha hali ya usafiri wa
reli
nchini, Mheshimiwa Mwakyembe pia amewaambia wananchi kuwa Wizara yake
pia
imeagiza crane mpya na kubwa ya kubebea mizigo yenye uzito unaofikia
kilo 100.
Kuhusu
injini za treni, Waziri Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete kuwa zabuni
kwa ajili
ya kutengeneza upya (re-manufacturing) injini nane za
treni imetolewa ili utengenezaji
huo ufanyike, iwe ni ndani ama nje ya nchi.
Pia
Waziri amesema kuwa oda imetolewa kwa ajili ya utengenezaji wa injini
mpya 13
za treni ambazo malipo yake yatafanyika katika mwaka ujao wa fedha hata
kama
utengenezaji wa injini hizo utaanza.
Aidha,
Waziri amesema kuwa Wizara kupitia mashirika yake hayo mawili imeagiza
spea za
kutosha kuweza kufanya ukarabati mkubwa wa injini tano kwenye karakana
zilizoko
hapa nchini.
“Mheshimiwa
Rais, kwa hesabu nyepesi tu ni kwamba katika kipindi kifupi tutaweza
kuwa na
injini kiasi cha 26 ambazo zitarudisha uhai wa usafiri wetu wa reli kwa
kiasi
kikubwa sana,” Waziri Mwakyembe amemwambia Rais
Kikwete.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
10
Januari, 2013
0 comments:
Post a Comment