Friday, January 11, 2013

JICHO LA ULIMWENGU WA HABARI KATIKA MAANDALIZI YA TAMTHILIA MPYA YA MY CAMPUS - UDSM

  1. Shumu Mwaita akifanyiwa make up kabla ya kuanza rasmi kushoot hook ya tamthiliya mpya itakayoruka kupitia Mlimani TV
  1. Hamadi Kimaya akiendelea na utaratibu wa make up ili kuanza kazi rasmi
Hapa vijana wakijadili jambo kuhusu  tamthiliya ya My Campus itakayokuwa ikiruka kupitia Mlimani TV

Muongozaji wa vipindi vya Televisheni na Filamu nchini Tanzania, Bw. Issa Mbura akitoa maelekezo kwa mpiga picha, Bw Emmanuel Kiwelu
Baadhi ya waigizaji katika Tamthilia ya My Campus wakijipumzisha

Assistant Production Manager  Catherine Allan (kushoto), akiwa na mwigizaji Sabina Shementse (Katikati) pamoja na Joyce Lyimo wakijipumzisha kidogo ili kuendelea na kazi.
DOP, Ochieng Gad Ogweno, Camera operator Emmanuel Kiwelu na Director Frank Mavura wakifuatilia kwa makini
Muigizaji Josephine Christopher akifanyiwa make up ili kuanza scene yake.
Mwakoba Kizaro atakayeenda kwa jina la Steven akiwa katika scene yake
Kazi ikiendelea kwa umoja na ushirikiano mkubwa
 
MAANDALIZI YA EPISODE YA 1
 Timu nzima ya MY CAMPUS ikiwa katika eneo la kazi Mikocheni ndani ya campus ya SJMC tayari kwa kupiga picha za episode #1
 Joyce na Emiliana wakifuatilia mchakato mzima wa upigaji picha za  My Campus.

  Neema, Silas, Mwakoba na Emiliana wakiwa katika scene kama wafanyakazi wa kazi za usafi katika Campus ya SJMC.
  Mtazamaji unachokiona katika picha hii si maigizo bali ni hali halisi inayowakumba wasanii tasnia ya filamu kwa ujumla, kwani mara nyingi vifaa huwa ni changamoto, lakini ubunifu huwa suluhisho la yote.



Director msaidizi Hawa (wa kwanza kulia) akiifuatilia kwa umakini moja ya scene.
 Mr Director Issa Athumani akikagua Kamera kuhakikisha kila kitu kinaenda sawia.
Atukuzwe (kushoto) na Glory (kulia) mojawapo ya wahusika wakuu katika mojawapo ya scene zitakazoonekana katika episode ya kwanza
 Moreen Swai aka Zawadi mhusika mkuu (kushoto), Edger Mahirane Production Manager na Shumu Mwaita wakiwa katika pozi la pamoja.
Moja kati ya wahusika wakuu Abdul Ibrahim aka Abdullah akiwa katika moja ya scene muhimu sana ili kuiunda episode ya Kwanza.
     Glory Swai akiwa makini na scene yake. Mambo mazuri zaidi yanatarajiwa kupitia Tamthiliya ya My Campus
 (Picha: Blog ya My campus)
 
Tamthiliya ya My Campus ni tamthiliya inayoandaliwa na wanafunzi wa jumuiya mbalimbali ambapo kwa kuanza imeanza na jumuiya ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na pia kusambaa kwenda vyuo vingine. 
 
Mwandishi mahiri wa mtandao huu wa ulimwenguwahabari.blogspot.com alipata fursa ya kujionea mwenyewe jinsi maandalizi ya Tamthiliya hii inayoandaliwa na wasomi wa chuo kikuu cha Dar es salaam, shule ya uandishi wa mawasiliano kwa Umma, ikiwa ni katika viunga vya Shule kuu ya Uandishi wa Habari na mawasiliano kwa Umma (SJMC) na kubaini kuwa ni kweli vijana wamedhamilia kuikomboa jamii kwa kuyaweka wazi mafunzo wanayoweza kuyapata kupitia maisha ya vyuo.
 
Tunawatakia kila la heri ndugu zetu wanaoiandaa tamthiliya hii na tunataraji itakuwa ni kazi ya kwanza Tanzania inayoangazia masuala ya vyuo hasa katika upande wa Tamthiliya

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI