SUALA la elimu ya Ukimwi
nchini limetakiwa kutiliwa mkazo kutokana na ugonjwa huo kuendelea kuwa tishio
kwa wananchi wengi wa Tanzania.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jipange Women Group Bi. Janeth Mavinza wakati wa kutoa huduma ya kupima Ukimwi eneo la Ujiji lililopo Mwananyamala, jijini Dar es salaam.
Bi. Janeth Mavinza Mwenyekiti wa Jipange Women Group akiongea na waandishi wa habari katika eneo la ujiji, Mwananyamala, jijini Dar es salaam. |
Bi. Janeth Mavinza
amesema licha ya wanawake hao kujishughulisha na ujasiliamali, pia wanatoa
msaada wa upimaji Ukimwi kwa hiari.
Kikundi hicho cha
Jipange Women kina asili ya VICOBA ambapo kimewakutanisha akina mama
wajasiliamali ili kuleta maendeleo ya kijamii.
Badhi ya wananchi waliojitokeza kushiriki katika mchakato huo |
Bi. Frola Mwakajinga - Katibu |
Bi. Frola Mwakajinga
kama katibu wa Jipange Women Group akaeleza umuhimu wa jumuiya hiyo, huku
akisisitiza wanawake kujiunga pamoja na kutatua matatizo yao kupitia vikundi
mbalimbali wanavyoviunda, lakini kikubwa ni kufanya kazi kwa bidii.
Wananchi nao
walijitokeza katika kupata huduma hiyo ya kupima kwa hiari huku wengi
wakizitaka taasisi nyingine za Afya kutoa huduma hiyo kwa watu waliopopembezoni
mwa mji kutokana na ukweli kwamba katika maeneo hayo huduma hii ni duni sana.
0 comments:
Post a Comment