Thursday, November 15, 2012

TCRA YATAKIWA KUELIMISHA JAMII JUU YA MOBILE NUMBER PORTABILITY

Mamlaka za mawasiliano na wadau mbalimbali wa mawasiliano Tanzania (TCRA) wametakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi wote kuhusiana na huduma mpya ya kutumia code moja kwa mitandao yote - MOBILE NUMBER PORTABILITY.




Prof Makame Mbarau akizungumza na waandishi wa habari katik katika mkutano wa kimataifa uliowakutanisha wadau toka nchi mbalimbali kujadili namna ya kutumia huduma hiyo mpya.

Katika kupiga hatua na kwenda na mabadiliko ya sayansi na tecknolojia Tanzania ipo katika mikakati madhubuti ya kutaka kutumia huduma mpya katika sekta ya mawasiliano kitaalam inafahamika kama MOBILE NUMBER PORTABILITY ambapo itawezesesha kutumia mitandao yote pasipo kubadilisha laini kama ilivyosasa.

Kutokana na kuwepo kwa mabadiliko hayo waziri wa sayansi na mawasiliano Proffesa Makame Mbarau amezitaka mamlaka husika kuhakikisha zinatoa elimu kwa wananchi ili kufahamu vyema huduma hii mpya, kwa kusema kuwa endapo zitatoa elimu kwa wananchi basi zitajenga uelewa na hatimaye huduma hii kueleweka na jamii kwa ujumla.


Wadau mbalimbali wakisikiliza kwa makini hoja zinazotolewa katika mkutano huo.

Tayari nchi nyingine zilizoendelea kisayansi na kiteknolojia zinatumia huduma ya MOBILE NUMBER PORTABILITY na sasa Tanzania imeanza mikakati kwa kushirikiana na nchi nyingine ili kuweza kutumia huduma hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI