Friday, November 9, 2012

TUME YA MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA YAOMBWA KUZINGATIA JINSIA

 Na Hilali Ruhundwa

TUME ya mchakato wa mabadiliko ya katiba mpya nchini imeshauriwa kutumia ripoti ya katiba na sharia ya chama cha sharia cha wanawake nchini ili kuzingatia masuala ya jinsia na haki zake.

Chama cha sheria cha wanawake Tanzania, kimeitaka tume ya mabadiliko ya katiba nchini, kuhakikisha kuwa inawashirikisha wananchi wote hasa wa vijijini, ili kutoa maoni ya ulingano wa kijinsia katika katiba hiyo.

Hayo yamebainishwa na mratibu wa jinsia wa chama cha sheria cha wanawake nchini Debora Mushi, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya katiba na sheria ya chama hicho, na kusema kuwa miongoni mwa mambo yaliyomo katika ripoti hiyo, yanaweza kutumiwa na tume ya mabadiliko ya katiba mpya, ili kutoa katiba yenye ulingano wa kijinsia.

Ameongeza kuwa haki zote za makundi hayo, ni muhimu ziingizwe ktk katiba mpya, ikiwemo haki za wanawake na makundi mbalimbali, sanjari na kuweka ukrasa maalum, unaoonesha utekelezaj wake.

Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ipo katika ukusanyaji wa maoni ya wananchi, kuhusu mchakato wa uundwaji wa katiba mpya, ambapo hivi karibuni, waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda, amesema kuwa zoezi hilo linaendelea vizuri, na kwamba kufikia mwaka 2014, itapatikana katiba mpya iliyotokana na wananchi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI