Na Emmy Mwaipopo
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB) imeagizwa kuhakikisha kuwa fedha zote zilizotengwa kwaajili ya mikopo kwa wanafunzi wanaondelea na masomo kupelekwa vyuoni leo (jana).
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, baada ya kuwepo kwa baadhi ya wabunge mbalimbali kuomba muongozo wa kutaka kujua ni jinsi gani serikali inaweza kuwasaidia wanafunzi waliokosa mikopo 2016/2017.
Suala hilo liliwekewa mkazo na mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete huku akieleza kuwepo kwa wanfunzi wa chuo cha UDSM kutaka kugoma kwa kukosa mikopo hiyo.
Aidha Ndalichako alisema kuwa fedha za mikopo kwaajili ya wanafunzi zilikwenda vyuoni wiki iliyopita.
“Tatizo lililotokea kwa UDSM sijui kama walidanganyana au laa!lakini hawakujaza fomu, serikali haitatoa fedha kwa mwanafunzi ambaye hajajaza fomu, waliosaini leo wataingiziwa fedha zao kwenye akaunti na vyuo,”amesema Ndalichako.
#Mwananchi
0 comments:
Post a Comment