Tuesday, November 15, 2016

WAHANGA WA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA KULAZIMIKA KUJENGA NYUMBA ZAO WENYEWE

Na EMMY MWAIPOPO
Serikali imewaomba wakazi wa mkoa wa Kagera walioathirika na tetemeko la ardhi kuendelea kujijengea wenyewe kwakuwa michango yote yenye thamani ya shilingi bilioni 5.4 iliyochangwa na wadau kwaajili ya kusaidia na walioathirika imeelekezwa kwa taasisi za serikali, na si wananchi binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu, alisema hadi sasa zimechangwa shilingi bilioni 5 na milioni 427. Alisema kamati ya maafa ya mkoa huo imeshatumia kiasi cha shilingi bilioni 1 na milioni 130 kukarabati miundombinu ya serikali iliyoathirika na kwamba fedha zilizobaki bilioni 4 na milioni 296 nazo zimeelekezwa huko.
Aidha aliwatoa wasiwasi wananchi waathirika wanaosubiri kupata msaada binafsi watalazimika kuchukua michango iliyotolewa na wadau wengine walioahidi kusaidia waathirika moja kwa moja na kwamba hata misaada hiyo ikipatikana watasaidiwa waathirika walio katika makundi maalumu kama wazee na walemavu.
“Fedha hizo ni kusaidia ujenzi wa wananchi waliobomokewa nyumba hususan kwa makundi maalumu ambayo ni wazee,walemavu,wagonjwa,wajane,wagane,wasiojiweza na yatima na wameomba kupatiwa orodha ya makundi hayo kwa awamu na awamu ya kwanza ni awamu ya watu 370 imeshawasilishwa ikiambatanishwa na picha za majengo yaliyobomoka,” alisema Kijuu.
Hata hivyo uamuzi huo wa serikali umepingwa vikali.
Tetemeko hilo la ardhi lilitokea September 10 mwaka huu na kusababisha madhara makubwa mkoani Kagera.
#CHANNEL 10

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI