Na Emmy Mwaipopo
MKE wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli aliyekuwa amelazwa katika hodi ya SiwejiHaji Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, ameruhusiwa na kurudi nyumbani Ijumaa hii.
First Lady huyo amewashukuru madaktari wote kwa matibabu waliompatia huku akiwashukuru watanzania kwa kumuombea.
“Nina mshukuru sana Mungu kwa kuimarisha afya yangu,pia napenda kuwashukuru wauguzi,nimepata huduma nzuri sana maana siku nilipoletwa hapa nilikuwa sina fahamu na hali yangu ilikuwa mbaya sana lakini mmenipigania na leo narudi nyumbani nikiwa na afya njema,”amesema Mama Janeth Magufuli.
Mama Janeth Magufuli alilazwa hospitalini hapo Novemba 9 mwaka huu baada ya kuugua ghafla na kupoteza fahamu.
0 comments:
Post a Comment