Friday, November 11, 2016

WAZIRI WA AFYA ASEMA SERIKALI HAINA TATIZO LA UHABA WA MADAKTARI HAPA NCHINI

WAZIRI wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Mhe Ummy Mwalimu imekiambia chama cha madaktari nchini-MAT-kuwa serikali haina tatizo la uhaba wa madaktari hapa nchni kutokana na vyuo vya udaktari vilivyopo kuzalisha zaidi ya madaktari elfu moja kila mwaka.
Akizungumza katika kongamano la mwaka la chama cha madaktari nchni Mhe Mwalimu amesema tatizo lililopo ni uwezo mdogo wa serikali kuajili wahitimu wote wa fani ya udaktari ambapo amesema katika madaktari elfu moja serikali inauwezo wa kuajiri madaktari mia tano tu.
Rais wa chama cha madaktari daktari Billy Haonga amesema kutokana na kauli ya serikali ya kutokuwa na fedha za kuajiri madaktari amewataka wataalamu kujadili tatizo la uwezo mdogo wa kifedha wa serikali pamoja na kutafuta fursa zitakazowawezesha kujiajiri ambapo pia ameitaka serikali kuweka mfumo wa bima kwa watanzania ili wawezesha kumudu gharama za matibabu ikiwemo kuonana na madaktari.
#ITV

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI