Saturday, June 21, 2014

DARAJA LA TABATA SEGEREA LILILOSABABISHA VIFO

picha
Na Lusajo, Tabata
DARAJA linalounganisha Majumba sita na Tabata Segerea limevunjika baada ya Lori kubwa kupita juu yake likiwa limebeba kontena kubwa wakati uwezo wa Daraja lenyewe ni Tani saba.
Inadaiwa kuwa watu watano wamepoteza maisha wawili wakiwa kutoka ndani ya Lori hilo na wengine kutoka gari iliyokuwa mbele ya Lori ambayo ilitumbukia wakati daraja likivunjika.
Daraja hilo lilifanyiwa matengenezo baada kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni na halikuwa limetengemaa kurejea katika hali yake ya kawaida.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI