Saturday, June 21, 2014

VALENCIA AIFUNGIA MAWILI ECUADOR IKIICHAPA 2-1 HONDURAS NA KUITUPA NJE KOMBE LA DUNIA

NI nina linalofahamika Valencia, lakini ni Enner na si Antonio anayetengeneza umaarufu wake katika Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ameingia katika orodha ya wachezaji wanaowania ufungaji bora baada ya kufunga mabao mawili usiku huu dhidi ya Honduras mjini Curitiba, Ecuador ikishinda 2-1.
Ameingia kwenye orodha ya wachezaji wanaotamba Ulaya kama Thomas Muller, Karim Benzema, Robin van Persie na Arjen Robben.
Lakini mshambuliaji huyo mwenye misuli na kasi, bado anacheza Amerika Kusini akiwa anachezea Pachuca ya Mexico, ingawa tayari timu za Ulaya zimeanza kumsaka.
Nyota: Valencia (kulia) akishangilia baada ya kufunga bao la pili katika ushindi wa 2-1 wa timu yake.
Ushindi huo unaipa pointi tatu Ecuador na kupanda hadi nafasi ya pili katika Kundi E ikiizidi kwa wastani wa mabao tu ya kufunga na kufungwa Uswisi, zote zikiwa nyuma ya Ufaransa yeny pointi sita, wakati Honduras haina pointi na inaendelea kushika mkia.
Ecuador itamaliza na Ufaransa ambayo imekwishafuzu ikihitaji ushindi kusonga 16 Bora wakati Uswisi itamaliza na Honduras ikihitaji ushindi pia- maana yake timu ya kuungana na mabingwa hao wa mwaka 1998 itajulikana siku ya mwisho ya mechi za makundi.
Mkali: Victor Bernardez (kushoto) akipambana na mshambuliaji wa Ecuador, Enner Valencia (kulia)

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI