Monday, April 28, 2014

LIVERPOOL HOI KWA CHELSEA, YAPIGWA MABAO 2-0

Demba Ba akiifungia Chelsea bao la 
kwanza dakika ya 45 ya mchezo.
Chelsea wakishangila bao lao la kwanza.
Liverpool hoi baada ya kipigo.
Willian akiifungia Chelsea bao
 la pili dakika ya 90.
 
Ba na Sakho wakichuana.
TIMU ya Liverpool imepokea kipondo cha bao 2-0 kutoka kwa Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa Uwanja wa Anfield jijini Liverpool.

Mabao ya Chelsea yamewekwa kimiani na Demba Ba dakika ya 45 wakati la pili likifungwa na Willian dakika ya 90.

Kwa matokeo hayo, Chelsea wamefikisha pointi 78 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 36 wakati Liverpool wakibaki kileleni na pointi 80 wote wakisalia na mechi mbili kumaliza ligi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI