Friday, November 4, 2016

ALI KIBA - 'HAKIWEZI KUNIKUTA KILICHOMKUTA DAVIDO SONY MUSIC'

Yapata miezi miwili sasa tangu tuzisikie taarifa za msanii mkali kutoka Nigeria Davido kutoa malalamiko kwa uongozi wa lebo ambayo inasimamia kazi zake kwasasa #Sony Music.

Malalamiko hayo yalitokana na kilichosemekana kuwa uongozi huo unamzuia msanii Davido kuachia kazi mpya bila kujali kuwa ni kipindi kirefu kimepita kwa msanii huyo bila kutoa kazi mpya.

Kutoka Bongo Flevani msanii @officialalikiba naye pia yupo chini ya uongozi huo wa Sony Music. Ila yeye ameiambia Perfect255 kuwa jambo kama lile lililomtokea Davido yeye haliwezi kumkuta kutokana na mkataba wake ambao amesaini na kampuni hiyo.

Ni baada ya kuulizwa kuwa yeye amejipanga vipi kama endapo litatokea kama lililomtokea msanii mwenzake Davido katika lebo hiyo. “Nimejiandaa vizuri, na pindi unapokuwa unasaini kitu ina maana kuwa umekubaliana na kila kitu, kwahiyo mimi pia nina matakwa yangu na hata wao pia wana matakwa yao, kwahiyo kitu ambacho kipo hapo ni kwenda na agreement. Me siwezi kukaa muda zaidi ya miezi 3 bila kutoa ngoma, na huo ndio mkataba wangu jinsi unavyosema.” Hayo ndio yalikuwa majibu ya Aikiba.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI