Monday, September 7, 2015

WAKAZI WA ILALA WATAKIWA KUWAAMINI UKAWA NA KUWAACHIA JIMBO


Muslim Hassanali, Mgombea ubunge jimbo la ilala kwa Tiketi ya CHADEMA na kuungwa mkono na UKAWA
STORY NA OPTATUSY STAN-DAR ES SALAAM
******
Wakati kampeni za uchaguzi mkuu zikiwa zimepamba moto katika maeneo mbalimbali nchini chama cha Demokrasia na maendeleo chadema katika manispaa ya ilala kimewataka wakazi wa manispaa hiyo  kukipa ridhaa ya kumchagua mbunge wake anayekiwakilisha ili kiweze kuwaletea maendeleo.

Hayo yamesemwa na mzamini wa chama hicho Bw Alkado Ntagazwa wakati wa mkutano wa chama hicho wa kumnadi mgombea wa  chadema anayeungwa mkono na umoja wa vyama vinanyounda ukawa Bw HASSANARI maarufu kama ROFA WA ILALA  uliofanyika katika viwanja vya soko la karume jijini Dar es salam,

Bw ntagazwa amesema kuwa wananchi wa eneo hilo hawapaswi kukosea tena na kukichagua chama cha mapinduzi kwa kuwa kimewaletea umasikini mkubwa ambao wanauona hadi sasa.Bw ntagazwa aliwambia wakazi wa eneo hilo kuwa miaka ya nyuma elimu ilitolewa bure kwa watu wote kwanini isiwe sasa? Bw ntagazwa alihoji.

Ntagazwa amewaomba wakazi wa manispaa ya ilala kutokosea kama ambavyo uwa wanafanya miaka mingine.Kwa upande wake mwenyekiti wa  wa vijana wa chama cha chadema Bw mwita amesema kama wananchi wa eneo hilo wataamua kukipigia kura chama chake katika nafasi zote watakuwa wamejiondoa kwenye matitizo mabalimbali kama kitendo cha kufukuzwa mara kwa mara na mgambo wa jiji kwenye maeneo yao ya kufanyia shughuli zao.

Mwita alibainisha kuwa watanzania wengi wana maisha magumu huku akiwataka polisi waache kutumika na badala yake wasimamie kanuni na taratibu za utekelezaji wa majukumu yao tofauti na ilivyo sasa Kwa upande wake mgombea wa ubunge wa jimbo hilo bw Hassanari amesema kuwa uwa anajisikia vibaya sana pale anapoona kuwa wakazi wa emeo hilo wananyanyasa na mgambo wa jiji huku wakiwa na uhalali wa kuishi kwa uhuru na haki katika maeneo yao.

Bw Hassanali ameongeza kuwa jambo la kwanza atakalolifanya kama atapewa ridhaa na wana ilala ni kuhakikisha kuwa fedha za maendeleo zinawafikia walengwa bila kuguswa na wajanja wachache.Huku akishangiliwa na wafanyabiashara na wananchi waliohudhuria mkutano huo bw hassanari alijinasibu kuwa yeye ndo muarobaini wa matatizo yote ya wakazi wa eneo hilo hivyo wana ilala hawakiwi kufanya makosa tena katika uchaguzi wa mwaka huu

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI