Friday, January 2, 2015

BREAKING NEWS: WANAHARAKATI WATEMBEA ZAIDI YA KILOMETA 1000 TOKA GEITA MPAKA DAR KUONANA NA RAIS KIKWETE *PICHAZ/VIDEO*

Vijana wa watatu wa kitanzania wametembea kwa miguu kwa muda wa mwezi mmoja kutoka Geita mkoani Mwanza kuja jijini dar es salaam kwa lengo la kukutana na rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya kikwete kumueeleza kilio chao dhidi ya mustakabali wa nchi.
Ni vijana wa watatu wakitembea mwendo wa zaidi ya kilometa eflu moja kutoka Mkoani Geita safari waliyoianza mnamo tarehe 24\11\2014  kuelekea dar es salam kumuona rais kikwete,
Vijana hao wameungwa mkono na baadhi ya vijana njiani baada ya kuwaona wakitembea huku wakidai kuwa wanamambo manne ya kumweleza rais  ambayo ni Rasilimali,Haki za binadamu,Rushwa na Ufisadi,
Vijana hawa wamepokelewa na jeshi la polisi  mara baada ya kupita katika wilaya ya kinondoni wakielekea ikulu ambapo wamehojiwa na mkuu wa wilaya kwa zaidi ya saa 3 huku vyombo vya habari vikizuiliwa kushuhudia mahojiano hayo,lakini baada ya muda mkuu wa wilaya akazungumza na waandishi wa habari huku akiwataka vijana hao kutoendelea na zoezi hilo kwa madai kuwa wamevunja sheria.
Angalia video hii hapa chini, kijana mmoja akieleza sababu yao kufanya hivyo.
Tafadhali endelea kuwa nasi tukujuze zaidi juu ya tukio hili.
LIKE PAGE YETU KUFUATILIA MATUKIO ZAIDI.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI