Monday, January 12, 2015

BONGO MOVIE JIFUNZENI HAPA: FILAMU ILIYOTENGENEZWA MIAKA 12 YASHINDA TUZO ZA GOLDEN GLOBE

FILAMU ya Boyhood iliyotayarishwa kwa muda wa miaka 12, ikiwa na washiriki hao hao, imeshinda tunzo za filamu za Golden Globe katika kipengele cha Best Drama film nchini Marekani.
Filamu ya Boyhood, ilijipatia ushindi mwishoni mwa wiki iliyopita, katika tunzo za Golden Globe, ambapo pia watu maarufu katika tunzo hizo walionyesha mshikamano na nchi ya Ufaransa, baada ya shambulizi lililofanyika jijini Paris.
Filamu hiyo imejinyakulia tunzo za Globes tatu, ikiwemo ya filamu bora ya kuigiza, muongozaji bora wa filamu hiyo ambaye ni Richard Linklater, tunzo ambazo zimefanyika katika hoteli ya Beverly Hilton mjini Los Angeles nchini Marekani.
Filamu hiyo inayozungumzia ukuaji, kutoka kuwa mtoto hadi utu uzima, pia muigizaji wake Patricia Arquette ameshinda tunzo ya muigizaji bora wa kushirikishwa.
Tunzo zingine zimeenda kwa muigizaji kutoka Uingereza Eddie Redmayne, ambaye ameshinda tunzo ya muigizaji bora katika ushiriki wake kama profesa wa fizikia katika filamu ya The Theory of Everything.
Kama zilivyo tunzo za Oscars, ambazo hupigiwa kura na wajumbe wa tasnia ya filamu takriban elfu sita, Tunzo za Globes nazo zinapigiwa kura na idadi ndogo ya waandishi wa habari 100 kutoka jumuiya ya vyombo vya habari vya nje vilivyopo Hollywood.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI