Kuna taarifa zilizoenea kuanzia jioni ya leo
January 10 kupitia mitandao mbalimbali, watu wametumiana picha na
taarifa kwamba Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amepata ajali.
Picha zilizoenea zinaonyesha Mbunge huyo amesimama na watu kadhaa pembeni ya gari aina ya Land Cruiser iliyopinduka.
Taarifa ya uhakika niliyoipata kuhusu
tukio hilo ni kwamba Mbunge huyo amepata ajali akiwa na wenzake wanne
ndani ya gari wakitoka Mbeya kuelekea Dar, ajali hiyo imetokea eneo la
Kitonga, Iringa eneo ambalo lina kona kali za barabara.
Taarifa iliyoandikwa na mwandishi Francis Godwin kwenye matukiodaima.co.tz imesema
hakuna mtu aliyefariki wala kupata majeraha makubwa ila Mbunge huyo ana
michubuko midogo midogo, Kamanda wa Polisi Iringa, Ramadhani Mungi
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Nafanya jitihada za kumtafuta Mbunge huyo, kwa taarifa zaidi endelea kutembelea ULIMWENGU WA HABARI
0 comments:
Post a Comment