MSANII wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ‘Mama Kijacho’ amefunguka kuwa, licha ya ujauzito wake kuwa mkubwa, mume wake Sunday Demonte hana taarifa yoyote juu ya kitumbo hicho.Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Aunt alisema maneno hayo yanaweza kuwashangaza watu lakini ndiyo ukweli wenyewe.
Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ‘Mama Kijacho’.
Alidai kuwa yeye na mume wake huyo hawajaachana na hajapewa talaka kama watu wanavyodai lakini hajui kwamba ni mama mtarajiwa na hata akijua hawezi kumuacha.
“Kiukweli mume wangu hajui kuwa nina ujauzito na hata akijua wala hawezi kuniacha, ananipenda sana. Sijaachana naye na wala sijapewa talaka, hayo yanayosemwa ni umbeya tu,” alidai Aunt.
0 comments:
Post a Comment