Thursday, December 25, 2014

ANGALIA NAFASI MPYA ZA AJIRA SERIKALINI ZILIZOTANGAZWA...CHEKI HAPA!

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TANGAZO LA KAZI
Serikali inatangaza nafasi za kazi ya Mafundi sanifu wa Maabara na Mafundi Sanifu wa Maabara Wasaidizi kwenye shule za Sekondari na Vyuo vya Ualimu, Tanzania Bara.
NAFASI; FUNDI SANIFU WA MAABARA WA SHULE/VYUO DARAJA LA II, NGAZI YA MSHAHARA TGTS C.1 (TSH.460,000)

SIFA ZA MUOMBAJI
1. Awe ni Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 45
2. Awe amehitimu kidato cha IV au cha VI na kufauru masomo ya Sayansi
3. Awe amepitia na kufuzu mafunzo ya miaka (3) na kutunukiwa cheti cha ufundi Sanifu (Full Technician Certificate-FTC) au Stashahada ya Kawaida (NTA Level 6) katika fani ya Maabara kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
4. Awe tayari kupangiwa kazi katika shule yoyote ya Sekondari au chuo cha Ualimu Ndani ya Tanzania Bara.

UTARATIBU WA KUWASILISHA MAOMBI
Maombi yakiwa na picha ya muombaji, nakala za cheti cha kuzaliwa, cheti cha kumaliza kidato cha nne, VI au stashahada yawasilishwe kwa mojawapo ya anwani zifuatazo;
Katibu mkuu
OWM-TAMISEMI
S.L.P 1923
DODOMA
AU
katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi Tanzania
S.L.P 9283
DAR ES SALAAM
Kwa wale wote ambao wamemaliza kidato cha IV na cha VI ambao walisoma masomo ya Sayansi na kufaulu katika Daraja A-C na ambao wapo tayari kupatiwa mafunzo maalum ya kuweza kupata sifa za kuwa Mafundi Sanifu wa Maabara au Mafundi Sanifu wa Maabara Wasaidizi, na wanapenda kuajiriwa, wanaweza kutuma maombi yao pia kupitia anwani zilizotajwa hapo juu.
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tar 20/01/2015
SOURCE; MWANANCHI 24TH DEC 2014.
=============

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TANGAZO LA KAZI
Serikali inatangaza nafasi za kazi ya Mafundi sanifu wa Maabara na Mafundi Sanifu wa Maabara Wasaidizi kwenye shule za Sekondari na Vyuo vya Ualimu, Tanzania Bara.

NAFASI; FUNDI SANIFU WA MAABARA WASAIDIZI WA SHULE/VYUO, NGAZI YA MSHAHARA TGTS B.1 (TSH.370,000)
SIFA ZA MUOMBAJI
1. Awe ni Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 45
2. Awe amehitimu kidato cha IV au cha VI na kufauru masomo ya Sayansi
3. Awe amepitia na kufuzu mafunzo ya Ufundi Stadi ngazi ya III (NVA Level III) katika fani ya Maabara kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
4. Awe tayari kupangiwa kazi katika shule yoyote ya Sekondari au chuo cha Ualimu Ndani ya Tanzania Bara.
5. Kwa Yule ambae ana stashahada za sayansi/ufundi ambayo siyo ya maabara awe tayari kupata mafunzo maalumu program ambayo itaandaliwa na NACTE kwa ajili hiyo.
UTARATIBU WA KUWASILISHA MAOMBI
Maombi yakiwa na picha ya muombaji, nakala za cheti cha kuzaliwa, cheti cha kumaliza kidato cha nne, VI au stashahada yawasilishwe kwa mojawapo ya anwani zifuatazo;
Katibu mkuu
OWM-TAMISEMI
S.L.P 1923
DODOMA
AU
katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi Tanzania
S.L.P 9283
DAR ES SALAAM
Kwa wale wote ambao wamemaliza kidato cha IV na cha VI ambao walisoma masomo ya Sayansi na kufaulu katika Daraja A-C na ambao wapo tayari kupatiwa mafunzo maalum ya kuweza kupata sifa za kuwa Mafundi Sanifu wa Maabara au Mafundi Sanifu wa Maabara Wasaidizi, na wanapenda kuajiriwa, wanaweza kutuma maombi yao pia kupitia anwani zilizotajwa hapo juu.
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tar 20/01/2015
Chanzo: MWANANCHI 24TH DEC 2014.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI