TAKWIMU za Maombi kwa watumiaji wa serikali katika mtandao wa kijamii wa facebook nchini marekani zimepanda kwa asilimia 24 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu ukilinganisha na miezi sita iliyopita.
Takwimu hizo zimekuja baada ya mtandao huo kufanya marekebisho ya tuhuma za kuvuja kwa siri za baadhi ya wateja katika kipindi cha hivi karibuni.
Kampuni hiyo inasema kuwa takwimu za maombi ya watumiaji wa serikalini duniani nzima zimepanda kwa asilimia 24 huku kiwango cha maudhui yaliyo zuiliwa kutokana na sababu za kisheria katika nchi husika zikipanda kwa asilimia 19.
Habari za kupanda kwa takwimu hizo zimekuja baada Facebook kukumbana na amri ya mahakamani ya kukabidhi takwimu za watu zaidi ya 400 na kuitaka ipeleke picha, ujumbe mfupi na maelezo mengine katika kesi ya udanganyifu.
Facebook inasema kuwa wamekuwa wakiangalia kila ombi la kutoka katika ofisi ya serikali na kulifanyia uchunguzi kubaini mapungufu yaliyopo.
Mark Zuckerberg
Mwezi April mwaka huu muanzilishi wa mtandao huo Mark Zuckerberg alianzisha kipengele kipya kinachoruhusu watumiaji wa mtandao huo kupunguza baadhi ya taarifa binafsi.
0 comments:
Post a Comment