Wednesday, November 5, 2014

RAIS ENRIQUE PENA NIETO APONGEZA KUKAMATWA KWA MEYA WA IGUALA, MEXICO *PICHAZ*

RAIS wa Mexico Enrique Pena Nieto amepongeza kazi nzuri ya waendesha mashtaka na majeshi ya usalama. Kwani Polisi wa nchi hiyo wamefanikiwa kumkamata meya wa mji wa Iguala, pamoja na mke wake ambako wanafunzi 43 walipotea mwezi Septemba.
Hata hivyo pena Nieto hakusita kufafanua matumaini yake kuwa kukamatwa kwao kutafumbua mambo mengi ambayo yana chunguzwa na waendesha mashitaka wa serikali.
Bwana Abarca na mkewe, Maria de los Angeles Pineda.
Amri ya kukamatwa kwa Bwana Abarca na mkewe, Maria de los Angeles Pineda, Ilitolewa baada ya maafisa wa polisi wa mji wa Iguala kusema walipewa amri kutoka kwa meya wa mji huo kupambana na wanafunzi.
Maafisa hao wanasema waliambiwa kuwazuia wanafunzi wasivuruge hotuba ya mkewe Bi Pineda katika mji wa Iguala siku hiyo.
Abarca.
Jose Luis Abarca ambaye amekuwa akitafutwa amekamatwa na maafisa wa polisi katika mji mkuu wa Mexico, Mexico City,  Na anatuhumiwa kwa kuwaamrisha polisi kupambana na wanafunzi katika siku ya kutoweka kwao tarehe 26 mwezi Septemba.

Wanafunzi hao kutoka chuo jirani cha mafunzo ya Ualimu, walisafiri kwenda Iguala kuandamana. Tangu siku hiyo hawajaonekana tena. Harakati za kuwatafuta wanafunzi hao kulifichua uwepo wa makaburi ya pamoja katika eneo hilo, lakini majaribio ya kwanza yalionyesha kuwa si ya wanafunzi.A

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI