Thursday, November 6, 2014

SOMA KUHUSU GADNER G HABASH KUMFIKISHA KOMANDO JIDE MBIBO MAHAKAMANI

******
MTANGAZAJI aliyetua Radio E-FM hivi karibuni akitokea Radio Times FM, Gardner G Habash ‘Kapteini’ anadaiwa kumpandisha kortini mkewe, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ kisa kikisemekana ni mgawanyo wa mali hivyo anataka haki yake baada ya kuwepo kwa madai mazito ya ndoa yao kuvunjika.
Mke wa Gardner G Habash, Judith Wambura Mbibo, ‘Lady Jaydee’ akipozi.
Kwa mujibu wa madai hayo, inasemekana kwamba Gardner amekimbilia mahakamani akidai apewe talaka na waweze kugawana mali walizochuma wote  ili kila mmoja achukue hamsini zake.
Chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa familia hiyo kililiambia gazeti hili kwamba, siku chache baada ya kutengana na huku hali ikizidi kuwa mbaya, mtangazaji huyo alichukua hatua ya kutafuta msaada kwa wanasheria.
“Msinitaje jina ila ninachowaambia ni kwamba Gardner tayari ameshampata mwanasheria anataka kumshitaki Jaydee.
“Anachohitaji ni kugawana mali zao, kila mtu afanye maisha yake na ukiangalia tu Gardner hana mpango tena wa kuendelea na maisha ya ndoa na Jaydee ila Jide yeye bado ana matumaini ya kurudiana wawe pamoja na hasa kinachomuuma ni kugawana mali

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI