Wednesday, November 5, 2014

SUDAN KUSINI INAKABILIWA NA UWEZEKANO WA KUWEKEWA VIKWAZO VYA UMOJA WA MATAIFA

Sudan Kusini inakabiliwa na uwezekano wa kuwekewa vikwazo vya Umoja wa Mataifa kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimedumu kwa miezi 11.
Ubalozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa umesema utasambaza rasimu ya azimio la vikwazo hivyo mnamo siku chache zijazo.
Afisa wa ubalozi huo ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar, hawana budi kuendelea na mazungumzo yanayo dhaminiwa na viongozi wa nchi za kanda ya mashariki mwa Afrika. 
Tangu mwezi May, Marekani iliwawekea vikwazo baadhi ya watu binafsi wanaohusika katika mgogoro wa Sudan Kusini.
Mapigano yaliibuka nchini humo Desemba mwaka jana katika taifa hilo changa ambalo lilipata uhuru mwaka 2011.
Duru zinasema watu zaidi ya watu 10,000 wamekwisha poteza maisha yao katika vita hivyo, huku mamilioni wakilazimika kuyahama makazi yao.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI