Wednesday, November 5, 2014

AJABU… SIKU HIZI MBWA WANA HOTEL ZAO, CHEKI HAPA WAKIFANYA MAMBO UFANYAYO BINADAMUA UKIWA HOTELINI *PICHAZ*

HOTELI ya kifahari ya wanyama nchini Singapore iliyozinduliwa hivi karibuni imeleta dira mpya kwa wananchi nchini humo kuwatunza, kuwafariji na kuongeza ukarimu kwa wanyama.
Hoteli hiyo maarufu kama Washngton hotel imekuwa ikitoa huduma za kulala, saluni na chakula kwa wanyama aina ya mbwa.
Washngton Hotel ni moja katika hotel za kifahari nchini humo yenye huduma za vyumba vyenye kiyoyozi murua huku ikitoa huduma za kuogela na chakula kwa wageni maalumu ambao ni wanyama aina ya mbwa.
Vyumba katika hoteli hiyo hugharimu kiasi cha dola 271 kwa usiku mmoja kwa mbwa watatu kuishi pamoja katika chumba chenye Television, kitanda na makochi ya ngozi.
Mbwa huogelea ndani ya bwawa la kuogelea wakiwa wamevalia boya, nguo maalumu kwa ajili ya maji wakiogelea kwa pamoja huku wakisaidiwa na wahudumu wa hoteli hiyo.
Mbwa hao hawaishii kwenye maji tu kwani hata huduma za saloon hushiriki ambapo mgunduzi wa hotel hiyo anasema kuwa wanastahili kuishi maisha haya.
Anasema kuwa, "hotel hii imebuniwa mahususi kwa ajili ya mbwa tu ingawa hata paka pia huwapokea lengo ni kuendeleza upendo kwa wanyama".
Na hata Mmiliki wa mbwa pia huweza kupata baadhi ya huduma pale anapowaleta mbwa wake kupumzika kama utengenezaji kucha, kusafisha sura na huduma zingine.

Mbwa akiwa amepozi kitandani.

Mmoja kati ya wafanyakazi wanaowahudumia mbwa hao akimpa sapoti mbwa wakati wa kuogelea.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI