HAYAWI Hayawi sasa yamekuwaaa...Hivyo ndivyo vifijo na nderemo zilizotawala mitaa ya Mwanza siku ya jumamosi Tar 22/11/2014 pale kijana mwanadiplomasia na mtoto anayetoka katika familia ya Mhe.Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chrispine Mizengo Pinda Alipoamua kuvunja ukimya na kumvisha pete mchumba wake wa siku nyingi Adelyne John Ngugi..
Bw.Chrispine Pinda ambaye amejiajiri na ni Msomi wa Post Graduate Diploma in Management of Foreign Relations (PGD-MFR) pamoja na mkewe mtarajiwa wote wamemaliza chuo cha kimataifa cha diplomasia (CFR) pamoja na Mkewe mtarajiwa bi Adelyne wamevishana pete na kuomba wadau wote wakiwemo marafiki wa karibu kuwaomea ili waweze kufikia malengo yao..
Mkurugenzi wa mtandao wa Ulimwengu wa Habari na uongozi wa mtandao huu, tunawatakia kila la kheri na afya njema hatimaye waweze kufikia siku ya kufunga pingu za maisha katika tukio linalotarajiwa kufanyika mapema mwakani jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment