Msanii wa muzikiwa Hip Hop nchini, One Incredible
LICHA ya baadhi ya wanamuziki nchini Tanzania kutangaza kuacha kutoa albamu za muziki kwa kile kinachoelezwa kutokuwa na faida, hali ni tofauti kwa Msanii wa muziki wa kufokafoka nchini Harry Kaale Maafuru kama One Incredible ambaye anasema kuwa albamu kwake ni kipimo cha usanii bora.
One Incredible ni moja kati ya wanamuziki wachache wanaofanya muziki wa kufoka foka nchini ambao wamekuwa na utamaduni wa kuendelea kutoa albamu licha ya baadhi ya wanamuziki kama vile Diamond, Roma mkatoliki, duly syskes na Mr Blue kunukuliwa kusitisha kutoa albamu kwa minajili ya kutokuwa na faida ikilinganishwa na kutoa wimbo mmoja mmoja.
Mwanamuziki huyo anasema pamoja na kuwepo kwa changamoto hiyo , kwa upande wake albamu ni muhimu na ndio kipimo cha kuonesha usanii wake na ndio maana anaendelea kutoa albamu.
Anasema kuwa kinachomtambulisha msanii katika jamii ni albamu yenye ubunifu na mkusanyiko wa nyimbo nyingi .
Incredible anatarajia kutoa albamu ya pili inayoitwa Representing Africa Popote Mwezi December mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment