Kanali Birocho Nzanzu
MAHAKAMA ya kijeshi Mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasi ya Congo imemhukumu kifo Kanali Birocho Nzanzu baada ya kubainika na makosa ya kutaka kumuua afisa wa jeshi la nchi hiyo.
Nzanzu anatuhumiwa kwa kosa la kutaka kumuuwa afisa aliyekuwa mstari wa mbele kutokomeza wapiganaji wa M23.
Afisa huyo anayedaiwa kupangiwa njama za kuuawa ni Mamadou Ndala ambaye kwa kiasi kikubwa aliamini katika vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa M23 na aliuawa mwezi Januari mwaka huu.
Afisa aliyeuawa Mamadou Ndala.
Hata hivyo hukumu hiyo imetolewa kwa watuhumiwa nane ambapo kati ya hao mmoja ndiye Kanali Nzanzu aliye hukumiwa kifo.
Mahakama imebainisha kuwa Kanali Nzanzu amekuwa akitumiwa na waasi wa ADF kutoka Uganda kwa kuandaa mauaji hayo.
Wakati huo huo shirika la kutetea haki za binadamu Hii leo limesema kwa miezi mi 3 polisi waliwaua wanaume na vijana wasiopungua 51, wakati mwingine wakiwa bila silaha, nje ya nyumba zao au katika masoko.
Watano kati yao walikuwa na umri kati ya miaka 14 hadi 17 na watu karibu 36 walitoweka na hawajulikani waliko.
Shirika hilo limewatolea mwito wafadhili wa kimataifa na Umoja wa Mataifa kuishinikiza Congo iwakamate na kuwafungulia mashataka maafisa waliohusika na mauaji hayo.
0 comments:
Post a Comment