Waziri Mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed
MAWAZIRI 14 wa baraza la mawaziri la serikali ya Somalia wametia saini taarifa inayotaka Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdiweli Sheikh Ahmed ajiuzulu.
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud
Mawaziri hao wanasema kuwa, mizozo na mivutano mikubwa baina ya Waziri Mkuu na Rais Hassan Sheikh Mohamoud ndiyo sababu iliyowasukuma watoe ombi la kujizulu waziri mkuu.
Mawaziri hao wanaamini kwamba, kujiuzulu Waziri Mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed ndiyo njia pekee ya kutatua mushkeli wa sasa wa hitilafu za uongozi katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Kabla ya Abdiweli, aliyekuwa Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon naye alilazimika kujiuzulu wadhifa wake huo miezi kumi na nne tu tangu alipochukua usukani huo baada ya kuzuka mivutano kati yake na Rais Sheikh Mohamoud.
Wachambuzi wa mambo wanaamini kwamba, kuna kibarua kigumu katika kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kisiasa ya Somalia.
Kutoeleweka vyema vipengee vya majukumu na mamlaka ya Rais na Waziri Mkuu ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kuwa sababu za kuibuka kwa hitilafu na mizozo ya kisiasa.
0 comments:
Post a Comment