Wednesday, November 19, 2014

FAMILIA YA BOB MARLEY KUUZA BIDHAA ZITOKANAZO NA BANGI *PICHAZ*

FAMILIA ya aliyekuwa mwanamuziki wa Jamaica, Bob Marley imezindua kampuni ambayo wanaitaja kama ya kwanza duniani kuuza bidhaa za Canbbisa.
Bob marley ni mwanamuziki aliyegusa hisia za wengi katika muziki wake wa Regge. Hivi sasa familia yake itauza bidhaa za Canbbisa au Marijuana au bangi kama inavyo julikana na wengi.
Bidhaa hizo zitajulikama kama 'Marley Natural' na na zitajumuisha mafuta ya urembo pamoja na manukato mengine ya wanawake na bidhaa nyinginezo.
Bidhaa hizo zitatengezwa na kampuni kubwa ijulikanayo kama Privateer Holdings iliyo mjini Washington Marekani, ikisisitiza kutaka kudumisha kumbukumbu ya mwanamuziki huyo aliyesifika kote duniani.
Mwanawe Bob Marley, Cedella Marley
Bidhaa hizo zitauzwa nchini Marekani na kwingineko duniani, Mwanawe Bob Marley, Cedella Marley, alisema hayati babake angekuwa hai angefurahishwa sana na wazo hilo. Kwani watu watajua uwezo wa majani ya bangi kutumika kama dawa.
Baadhi ya majimbo yana ruhusu utumiaji wa bidhaa hiyo kwa sababu za matibabu tu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI