MSANII wa kike maarufu nchini Marekani Nick Minaj amesema kuwa hana mpango wa kuolewa kwa sasa wala kuanzisha familia kwa sababu anahitaji kuwa mama bora kwa mtoto wake.
Anasema kuwa,hatopenda kuchanganya mambo yake ya familia na biashara ya muziki hivyo anatarajia kupata mtoto na kuolewa mara baada ya kumaliza albamu yake Tano.
Mkali huyo wa muziki wa kufoka foka nick Minaji anasema kuwa atakapokuwa na mtoto, atatumia muda mwingi kuwa nae, na hatopenda kuona watoto wake wahisi kama hawapi matunzo kwa umakini hivyo anatarajia kupumzika muziki kwa muda.
Msanii huyo kutoka familia ya Young Money anasema kuwa endapo atamaliza albamu yake ya tano bila kuwa na mtoto itamuhuzinisha kwani anadhani huo ndio muda sahihi kwake kuitwa mama ingawa hatarajii kuzaa kabla ya kuolewa.
Minaj alinaetamba na wimbo wa Anaconda kwa sasa, anasema kuwa suala la ndoa kwa ameliweka pembeni kwani ahitaji kuingiza watu kwenye biashara yake ya muziki, na anataka kila kitu kiwe na mpangilio kwake hivyo baada ya albamu ya tano ataweka muziki pembeni na kufanya yote hayo ikiwemo kupata mtoto wa kwanza na wa pili ikibidi huku akiwa na kiasi cha dola million 500.
Mpaka sasa ana album mbili huku akitarajiwa kutoa albamu ya tatu ThePinkPrint ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment