HUKU gharama ya ardhi ikizidi
kupanda, baadhi ya maeneo yaliosahaulika kama vile vyoo vya zamani yamegeuzwa
na kufanywa kuwa migahawa na maduka ya kuuza nguo.
Vyoo vingi vya kukojoa vilisahaulika kwa miongo kadhaa baada ya vita vya
dunia vya pili ,lakini kufuatia hatua ya maafisa wa jiji hilo la kutaka kupata
mapato, mabadaliko hayo yanafanyika kwa kasi.
Baadhi ya migawaha hiyo ni 'The Convinience' uliofunguliwa katika eneo la
Hackney mwaka 2013, 'WC' ambalo ni duka la mvinyo lililopo katika eneo la
Clapham kusini mwa London na 'ArtsLav' ambalo ni eneo la maonyesho lililopo
katika eneo la Kennington.
Vyoo
london kulingana na mtandao wa gazeti la daily nation kenya.
Kulingana na
mtandao wa gazeti la daily Nation nchini Kenya, Maeneo mengine yaliokuwa vyoo na
kugeuzwa ni 'the Attendant' na 'the Cellar
Door' cabaret lililopo katikati ya mji wa London.
Mwenendo huo
ulianza hivi majuzi kulingana na Rachel Erickson ambaye kazi yake ni kupanga mipango ya watalii kuzuru
katika vyoo hivyo hatua iliomsababisha kuitwa 'Mwanamke wa vyoo'.
Jayke Mangio
mwenye umri wa miaka 34,ambaye alifungua 'WC' mnamo mwezi July,amesema kuwa
serikali imekuwa ikilishinikiza baraza la jiji kutumia maeneo yote yalio wazi
kuleta mapato.
Baadhi ya maeneo ambayo yamevutia
wawekezaji ni vyoo hivyo vya zamani na barabara za chini za
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment