KIJANA mmoja mkazi wa Kimandolu
jijini Arusha, (jina kapuni) mwenye umri wa miaka 18 amelazwa katika hospitali
ya mkoa Mount Meru baada ya kubakwa na kisha kukatwa ulimi na mwanamke mmoja
aliyekuwa akimtaka kimapenzi.
Tukio hilo la kusikitisha
limetokea jana majira ya saa 6.30 usiku katika eneo la Tindigani, kimandolu,
wakati mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina moja la mama Abuu alipofika katika
bar hiyo kama mteja na baadaye alimlazimisha mhudumu wa bar hiyo ambaye ni
majeruhi kufanya mapenzi bila ridhaa yake.
Akiongea na mwandishi wa habari
hii mfanyakazi katika bar hiyo, inayomilikiwa na mwenyekiti wa mtaa ,Joel
Mbasha alisema mnamo majira ya usiku alikuja mwanamke huyo na kuagiza
kinywaji huku yeye akimhudumia kabla hajamgeuzia kibao.
Alieleza kuwa ilipotimu majira ya
saa 6.30 wateja waliisha katika bar hiyo na kuamua kufunga bar ,hata hivyo
mwanamke huyo ndiye aliyebaki pekee akinywa pombe taratibu katika eneo hilo
ndipo alipomlazimisha kufanya kitendo hicho ambapo alimziba mdomo kwa kutumia
kinywa chake na baadae alifanikiwa kumng’ata ulimi na kuutema chini.
Majeruhi huyo kwa sasa hali yake
bado mbaya kwani hawezi kuongea na muda mwingi anatokwa na damu nyingi hatua
ambayo imewalazimu wahudumu katika hospitali hiyo kumwekea ndoo ya kutemea
damu.
Jeshi la polisi mkoani Arusha
limethibitisha tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na upelelezi
utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
0 comments:
Post a Comment