Wednesday, October 15, 2014

HATARI TUPU: MNENGUAJI ASHA MADINDA ATEKWA DUBAI......TAZAMA ALICHOFANYIWA HAPA!

 
MNENGUAJI wa bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’, Aisha Ramadhani Mbegu maarufu kama ‘Aisha Madinda’, hivi karibuni anadaiwa kufanyiwa kitu mbaya baada ya kupokonywa pasipoti na simu zake kisha kubadilishiwa kazi aliyokusudia kuifanya  na kufanywa hausigeli.
Akisimulia mkasa mzima, Mkurugenzi  wa Aset, Asha Baraka alisema Aisha alikwenda nchini Dubai kwa lengo la kufanya shughuli za unenguaji, lakini aliyempokea alimbadilishia kibao kwa kumnyang’anya kila kitu ili asipate mawasiliano na baadaye kumfungia kwenye jengo moja na  kumfanyisha kazi za ndani.
Asha anayejulikana pia kama Iron Lady, aliendelea kuweka wazi kuwa baada ya Aisha kufanyiwa hivyo hakuwa tena na uwezo wa kuwasiliana na mtu yeyote zaidi ya waliomteka, ila yeye alipata habari hizo baada ya kuwauliza baadhi ya wasichana wanaofanya kazi huko waliomwambia kuwa tokea wawepo Dubai hawajawahi kumuona wala kusikia habari zake.
“Yaani walimpokonya hati za kusafiria, wakampeleka kufanya kazi za ndani katika majumba ya watu, nimeshamfuatilia kujua alipo na sasa tunafanya utaratibu wa kumrejesha nyumbani, inahitajika kama dola 800 (zaidi ya milioni 1)kwa ajili ya kulipia kibali cha kuishi alichokuwa amepitiliza,” alisema Asha Baraka.
Aisha aliondoka nchini hivi karibuni kwenda huko kwa ahadi ya kwenda kunengua katika kumbi mbalimbali za starehe, lakini ndoto zake zikayeyuka.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI