Na Musa Mateja
Tumetoka mbali! Picha ya staa wa Pozi kwa Pozi ‘PKP’, Omary Nyembo
‘Ommy Dimpoz’, aliyofotolewa enzi anaingia jijini Dar kwa treni imekuwa
kivutio kikubwa kwa mashabiki wake na sasa inaelekea kutapakaa kila kona
ya nchi na wengi wakibishana namna alivyokuwa awali na muonekano wake
wa sasa.
Huu ni muonekano wa Staa wa Pozi kwa Pozi, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kwa sasa.
Huu ni muonekano wa Staa wa Pozi kwa Pozi, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kwa sasa.
Picha
hiyo ambayo ameipiga kitambo juzikati ilisambaa kwa kasi kwenye
mitandao mbalimbali ya kijamii na kuwafanya watu waanze kubishana kama
ni yeye au ni mtu anayefanana naye na wengine kukerwa na picha hiyo
wakisema itolewe kwa kuwa inamdhalilisha staa wao.
Baada ya
kuona mzozo huo unakuwa mkubwa, gazeti hili lilimtafuta Ommy Dimpoz ili
aeleze kama ni yeye ambapo alikiri kwamba ni yeye na kudai aliyekuwa na
picha hiyo ni mjomba’ake tu anashangaa ilivyovuja mitandaoni.
Chanzo: GP
0 comments:
Post a Comment