Saturday, October 11, 2014

MVUA YAITIBUA NIGERIA KUSAKA TIKETI YA MOROCCO

TIMU ya Taifa ya Nigeria jana ijumaa ilishindwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Khartoum kujiandaa na mechi dhidi ya Sudan kutokana na uwanja kujaa maji kufuatia mvua kubwa kunyesha Khartoum, mji mkuu wa Sudan.
Super Eagles waliwasili mapema jana na walikuwa na ratiba ya kufanya mazoezi jioni, lakini ikashindikana kutokana na tatizo hilo.
Msemaji wa timu ya Taifa ya Nigeria, Ben Alaiya baadaye alikiri kuwa wanatarajia kuripoti suala hilo CAF.
Sudani na Nigeria sitachuana leo jumamosi katika mchezo wa makundi kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Africa mwakani nchini Morocco.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI