Saturday, October 11, 2014

MAUAJI YA KUTISHA NDANI YA KANISA LA PAG BUKOBA

Katika hali isiyo ya kawaida,watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wamevamia Kanisa la PAG tawi la Kagemu kata ya Kitendaguro manispaa ya Bukoba na kumua muumini mmoja kwa kumcharanga mapanga hadi kufa na mwenzake kujeruhiwa, hawakuiba chochote ikiwemo simu zao.
Hata hivyo tukio hilo linahusishwa na imani za kidini kwamba waliohusika na tukio hilo ni wapinzani ya dini yao.
Mtoa habari aliyegoma kutaja jina amesema chanzo cha mgogoro huo na kifo cha muumini ambaye ni mwalimu katika shule ya sekondari KAGEMU ni baada ya marehemu kuoa mwanamke wa dini nyingine (inaifadhiwa) na kumbadilisha dini huyo mkewe na hapo waumini wa dini ya mkewe walianza vitimbwi kwa kanisa hilo na hadi mauaji hayo kumekuwa na vurugu za kila mara baina ya pande mbili.
Polisi bado wanachunguza na watatoa taarifa baadae,mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha maiti bukoba mjini,majeruhi amelazwa hospital ya mkoa. 
Viongozi wa makanisa ya PAG walitarajiwa kutoa tamko rasmi mchana wa leo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI